Rais Omar al-Bashir, ameapishwa kwa muhula mwengine wa miaka mitano baada ya kupata ushindi mwengine kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika April.
Al- Bashir,angali na kesi na koti ya kimataifa ya ICC inayomtuhumu kwa mauaji yaliyofanywa dhidi ya baadhi ya wakaazi wa Darfur, nchini humo.
Kura hiyo ilisusiwa na vyama vya upinzani lakini ikaendelea licha ya wapiga kura wachache kujitokeza..
Viongozi wa Kenya , Misri na Zimbabwe ni baadhi ya waliohudhuria sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Al Bashir ambaye amekuwa madarakani tangu alipochukua hatamu za uongozi kupitia mapinduzi ya mwaka 1989.
No comments:
Post a Comment