Mwenyekiti wa shirikisho la soka nchini Liberia Musa Bility ametangaza mpango wake wa kutaka kuwania urais wa shirikisho la soka duniani FIFA akisema ni wakati wa Afrika kuongoza.
Afisa huyo mwenye umri wa miaka 48 ni mtu wa pili kutangaza azma yake ya kugombea wadhfa huo baada ya aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa timu ya Brazil Zico.
''Afrika ndio kundi kubwa katika FIFA kwa hivyo lazima tuchukue uongozi wa kuunganisha soka''.
''Sote tunakubali kwamba FIFA inakabiliwa na wakati mgumuna ni wakati mgumu ambapo viongozi hujitokeza''.
Bility ambaye ameliongoza shirikisho la soka nchini Liberia FA tangu mwaka 2010,ni Mwafrika wa pili kutaka kuwania urais wa shirikisho la soka duniani.
Rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF Issa Hayatou alipoteza kwa SEPP Blatter wakati wa uchaguzi wa FIFA mwaka 2002.
Mnamo mwezi Juni tarehe 2,Blatter mwenye umri wa miaka 79 alitangaza kwamba atajiuzulu kama rais wa FIFA kufuatia madai ya ufisadi yaliowakumba maafisa wa FIFA.
No comments:
Post a Comment