Mtu mmoja amechinjwa na mwengine akajeruhiwa vibaya baada ya shambulizi la kiislamu katika mji wa Lyon Ufaransa.
Vilipuzi kadhaa vilitegwa katika karakana moja iliyoko Saint-Quentin-Fallavier
Mvamizi aliyetekeleza mauaji hayo anasemekana kuwa alikuwa akipeperusha kibendera cha wanamgambo wa kiislamu.
Kibendera hicho kilipatikana kimetupwa karibu na eneo la tukio.
Mwanaume mmoja amekamatwa na maafisa wa usalama kufuatia tukio hilo.
Waziri wa usalama wa ndani Bernard Cazeneuve yuko njiani kuelekea kwenye eneo la tukio.
nza nWakati huohuo rais wa Ufaransa Francois Hollande anatarajiwa kukatiza ziara yake rasmi ya viongozi wa bara ulaya na kurejea nyumbani kukabili janga hilo.
Shambulizi hili ni la kwanza tangu lile la kigaidi lililopelekea kuuawa kwa watu 17 miezi sita iliyopita.
No comments:
Post a Comment