Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Stephen Ngatunga akiongea na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha na wawakilishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo aliipongeza serikali kupitia Mamlaka hiyo katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa mawakala wa forodha na kuiasa kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali katika sekta hiyo ili kuiwezesha serikali kupata mapato kwa maendeleo ya Taifa, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kulia ni Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi.
Mwanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) wakichangia wakati wa mkutano uliokutanisha Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Na
Hassan Silayo-MAELEZO
MAWAKALA wa Forodha nchini wameaswa kujisajili katika mfumo wa uondoshaji mizigo wa Himaya
moja ya Forodha ya Afrika Mashariki (Single Custom Territory) utakao anza
kutumika hivi Karibuni.
Hayo
yamesemwa na Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw.
Tiagi Kabisi wakati mkutano na Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa
Forodha (TAFA).
Bw.
Kabisi alisema kuwa mawakala wa forodha nchini hawana budi kufanya hivyo ili
kuwezesha uondoshwaji wa mizigo kwa haraka zaidi pindi mfumo huo utakapoanza
kutumika.
“Sasa
tunaelekea katika matumizi ya Himaya moja ya Forodha ya Afrika Mashariki yaani
Single Custom Territory ili kuwa na uwezo wa kupata huduma kwa kutumia mfumo
huo pindi matumizi yatakapoanza mapema ili kuondoa usumbufu utakaoweza
kutokea”. Alisema Bw. Kabisi.
Bw.
Kabisi aliongeza kuwa mpaka sasa ni makampuni mawili (2) ya mawakala
waliojisajili mpaka sasa.
Aidha
Bw. Kabisi alisema kuwa mawakala wa forodha hawana budi kuendelea kuwa waamifu
ili waendelee kuongoza katika makusanyo ya fedha kwa mwaka ujao ambapo kwa
mwaka huu wamechangia kwa asilimia 40 ya mapato ya serikali.
Naye
Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Stephen Ngatunga alisema kuwa
wataendelea kushirikiana na Mamlaka la Mapato Tanzania (TRA) katika kuhakikisha
wanaifanya idara ya forodha inafanya vizuri katika makusanyo ya fedha.
Pia
Bw. Ngatunga aliitaka serikali kuendelea kushughulikia changamoto mabalimbali
zinazoikabili idara hiyo ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu na kuendelea kuongoza
katika makusanyo ya mapato ya serikali.






No comments:
Post a Comment