Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitumia usafiri wa pikipiki alipokuwa anakwenda Kijiji cha Ilyamchele, Kata ya Namonge ambako aliendesha harambee ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Ilyamchele akiwa katika ziara wilayani Bukombe, Geita, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi cya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Msafara wa Komredi Kinana ukivuka katika moja ya mio iliyopo Barabara ya Ilyamchele.
Gari lililombeba Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye likivuka katika moja ya mito katika Kijiji cha Ilyamchele, wilayani Bukombe.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiakivuka kwenye daraja la Ilyamchele baada ya kuzindua ujenzi wa daraja hilo, wilayani Bukombe, Geita,akiwa katika ziara wilayani Bukombe, Geita, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi cya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Nape akivuka katika daraja bovu la Ilyamchele.
Watoto wakiwa karibu na chumba cha darasa cha Shulre ya Msingi Ilyamchele, katika Kata ya Namonge, wilayani Bukombe. Komredi baada ya kuona hali hiyo, aliitisha harambee ya ujenzi wa shule hiyo, isiyokuwa na walimu wataalamu.. picha zote na richard mwaikenda.

No comments:
Post a Comment