TANGAZO


Thursday, June 18, 2015

Kenya yamsaka mpiganaji wa Alshabaab

Raia wa Ujerumani anayesakwa
Maafisa wa polisi nchini Kenya wametoa zawadi ya dola laki moja kwa mtu yeyote atakayemkamata raia wa Ujerumani anayetuhumiwa kuhusika katika shambulizi la kundi la Alshabaab.
Andreas Martin Muller anadaiwa kuwa mmoja ya washambuliaji waliovamia kituo cha jeshi katika kaunti ya Lamu.
Wanamgambo 11 na wanajeshi wawili wa Kenya walifariki.
Raia mwengine wa Ulaya Thomas Evans kutoka Uingereza pia alishiriki katika uvamizi huo kabla ya kuuawa.

No comments:

Post a Comment