TANGAZO


Sunday, June 14, 2015

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimuweka tone la chanjo mtoto wa miezi sita Innocent Noel  wakati wa uzinduzi wa chanjo kwa watoto katika Zahanati ya Kashinja,Kata ya Nyakisasa, wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Akihutubia baada ya uzinduzi wa chanjo hiyo, Komredi Kinana aliwataka wananchi kuachana na tabia ya kutowapeleka watoto hospitali kupata chanjo kwa sababu zisizo za masingi za kuamini mambo ya kishirikina, kwani chanjo ni kinga ya uhakika ya magonjwa mbalimbali kwa watoto. Pia katika zahanati hiyo alizindua ujenzi wa nyumba ya Mganga.
Komredi Kinana akimpatia chanjo mtoto Lillian Vicent
Ngoma ya asili ikutumbuiza wakati wa mapokezi ya Komredi Kinana, alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Benaco, wilayani Ngara leo.
Komredi Kinana akiangalia ngoma ya asili ikitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha  Benaco Kata ya Kasulo, wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera.
Ngoma ya asili ikitumbuiza katika mkutano huo wa hadhara mjini Benaco.
Komredi Kinana akisoma taarifa ya aliyopewa wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ngara.


Komredi Kinana akisaidiana na baadhi ya viongozi kumpatia fundi bati aliposhiriki ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tawi ya CCM Munjewe, Kata ya Ruhende.
Komredi Kinana akisaidia kumtwisha ndoo ya maji Francisca Katana baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kata ya Rulenge, wilayani Ngara leo.

No comments:

Post a Comment