Aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Jack Warner amesema katika hotuba ya kushangaza aliyotoa katika runinga kwamba atafichua kila anachojua kuhusu ufisadi katika shirikisho hilo.
Bwana Warner ambaye alisema kuwa anahofia maisha yake pia amesema kuwa anaweza kuwahusisha maafisa wa FIFA na uchaguzi mkuu katika taifa la Trinidad and Tobbago mwaka 2010.
Ni mmoja wa watu 14 walioshtakiwa na Marekani kuhusiana na ufisadi katika FIFA.
Mmoja wa maafisa wakuu wa FIFA na shahidi muhimu Chuck Blazer alikubali kuchukua hongo.
Afisa huyo alikiri kufanya hivyo mnamo mwaka 2013,ikiwa ni miongoni mwa mashtaka yaliofunguliwa ambayo yameikabili FIFA na kumlazimu rais wake Sepp Blatter Kujiuzulu.
Idara ya mahakama ya Marekani inadai kuwa watu 14 walioshtakiwa walikubali hongo ya zaidi ya dola milioni 150 katika kipindi cha miaka 24.
Watu wengine wanne walikuwa tayari wameshtakiwa akiwemo Blazer.
No comments:
Post a Comment