Na Salma Ngwilizi MAELEZO
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili(MNH) iliyopo jijini Dares Salaam inatarajia kuanzisha huduma ya hospitali inayotembea kwa kutumia gari maalum mara baada ya kukakamilisha mchakato wa gharama za matibabu kupitia mfumo huo.
Hayo yalisemwa leo Dkt. Gimmy Temba kutoka Kitengo cha Dharura cha MNH na kwenye maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijijni Dares Salaam.
“ Tunamagari magari mawili ya hospitali inayotembea ambayo tunapata msaada kutoka nchi ya Japan yenye vifaa kisasa kwa ajili uchunguzi wa matibabu ya dharura wa mgonjwa ,” alisema.
Alisema hivi sasa wako katika mpango wa kuangalia namba maalum ambazo zitakuwa zinatumika wakati mgonjwa anapokuwa akihitaji huduma hiyo. Hivyo namba hizo zitakapo kuwa tayari watazitangaza kwa wananchi ili waweze kuzifahamu.
Aliongeza kuwamba magari ya hayo yako mawili nchi nzima na yatakuwa yanatoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa dharura, pia wanatarajia kupata magari mengine mawili .
Alivitaja baadhi ya vifaa vilivyoko katika magari hayo kuwa ni mashine ya kuangalia mzunguko wa damu na hewa, kusukuma damu,kupumzisha ikiwemo ya kuondoa uchafu mfano vile damu au mate.
TFDA: NUNUENI VIPODOZI KWENYE
MADUKA SALAMA KUEPUKA MADHARA
Na Salma Ngwilizi-Maelezo
WANANCHI wametakiwa kuhakikisha wananunua bidhaa za vipodozi kwenye maduka ambayo yamethibitishwa na Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) ili kueweza kuepuka madhara ya magonjwa mbalimbali ikwemo saratani.
Hayo yamesemwa leo na Afisa Muelimishaji wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Bw.James Ndege kwenye maadhimisho wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja.
“ Madhara ya vipodozi vilivyopigwa marufuku ni makubwa kuliko watu wanavyofikiria sasa watu wanafikiri kwamba yale madhara wanaweza kuona kwa siku moja lakini kumbe yale madhara yanaendelea kujikusanya kila unapoendela kutumia kipodozi kilichopigwa marufuku alafu mwisho ikishafika ile hatua yale madhara kuweza kuonekana ndo unaona mtu ameugua saratani anakwenda kwa daktari.”alisema Bw.Ndege.
Aidha alisema kuwa matumizi ya vipodozi hivyo uingiza sumu ndani ya ngozi ya binadamu pia madhara yake ni pamoja na saratani ya ngozi,ini,figo kuharibika,kupatwa na aleji ya ngozi (mabakabaka) na kuweza kusababisha kuzaa mtoto mwenye utindio wa ubongo, vilevile inaweza kusababisha kupoteza kumbukumbu.
Ndege aliongeza kwamba hivi sasa ili kuweza kuifanya jamii iweze kuepukana na matumizi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku TFDA wameanza kutoa elimu kwa wanafunzi za msingi ili waweze kuelewa na kuelimisha jamii juu ya madhara hayo.
No comments:
Post a Comment