Na Andrew Tangazo Chimesela (Morogoro)
0719
11 22 99/ 0785 336 335
18
Juni, 2015
Halmashauri
ya Wilaya ya Morogoro, imefanikiwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria
kwa asilimia 8 ukilinganisha na
maambukizi ya ugonjwa huo mwaka 2014.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Dkt. Mwanahamisi Yahya ambaye
ni Kaimu mganga wa kituo cha Afya cha Mkuyuni Wilaya ya Morogoro wakati akiwasilisha
taarifa ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge
Kitaifa, Ndugu Juma Khatib Chum.
Dkt. Mwanahamisi amesema, mapambano dhidi ya malaria Katika
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ni moja ya Kipaumbele kinachotiliwa mkazo na
Halmashauri hiyo kupitia Idara ya Afya, jitihada zilizoleta matokeo chanya ya
kushusha maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia Nane.
“Hali ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria katika Halmashauri
yetu imeshuka kwa asilimia Nane kutoka asilimia 56 mwaka 2014 hadi asilimia 48
mwaka 2015”, matokeo haya yametokana na
jitihada za Halmashauri ikishirikiana na wadau mbalimbali ”.aliongeza Dkt.
Yahya.
Dkt. Yahya amesema, Kituo cha Afya cha Mkuyuni na Zahanati
zilizopo katika Tarafa ya Mkuyuni vimeendeleza mapambano dhidi ya Malaria kwa
kutoa Elimu kwa akimama Wajawazito ili kuzuia maambukizi ya malaria kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto.
Jitihada nyingine zilizofanywa katika kupunguza mambukizi ya
Malaria kushirikiana na Wadau mbalimbali
ni pamoja na kuhamasisha jamii
kutumia kikamilifu vyandarua vilivyotiwa viwatilifu na kusafisha mazingira ili
kuondoa mazalia ya mbu wanaosababisha
malaria.
Aidha, Dkt. Yahya alitaja lengo la mapambano dhidi ya Malaria
kuwa ni kupunguza maambukizi, magonjwa
na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria katika jamii kwa kutoa Elimu na
huduma Bora za Afya kupitia vituo vya Afya na Zahanati.
Sambamba na Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Ndugu Juma
Khatib Chum kupokea Taarifa hiyo ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria, alifungua
nyumba ya mtumishi wa kituo cha Afya cha
Mkuyuni iliyojengwa kwa gharama ya shilingi 135,000,000.00.
Miradi mingine ya maendeleo iliyopitiwa na mwenge huo ni
pamoja na mradi wa utunzaji mazingira Kijiji cha Kiloka, mradi wa maji na usafi
wa mazingira wa Kijiji cha Changa na mradi wa Ufugaji bora wa nyuki uliopo
kijiji cha Kikundi.
Miradi mingine ya maendeleo iliyopitiwa na Mwenge huo ni
mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Mtego wa SImba, mradi wa mashamba ya
Kikundi cha Vijana wakulima wa mahindi na mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Vicoba
Kikundi cha Upendo.
Mwenge wa uhuru umeingia siku yake ya tatu kukimbizwa katika
Mkoa wa Morogoro ambapo leo umekimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya
Morogoro na kupitia miradi saba ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi
323,142,000.00.
No comments:
Post a Comment