MPANGO MBAYA ni filamu iliyochezwa na washiriki 10 waliofanikiwa kuingia katika Fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) msimu wa kwanza 2014 na kushirikisha baadhi ya waigizaji mahiri kutoka katika kiwanda cha Filamu Tanzania.
Filamu ya Mpango Mbaya ni filamu ambayo imetengenezwa kwa viwango vya hali ya juu huku ikikidhi viwango vya kimataifa na ni filamu ambayo ina ubora wa hali ya juu kuanzia ubora wa picha, Sauti, rangi mpangilio wa matukio na upigwaji picha wake na ubora wa washiriki wa filamu hiyo.
Filamu hii itazinduliwa mnamo tarehe 12 Juni 2015 Katika Ukumbi wa Mlimani City na pia Filamu hii itaendelea kuonyeshwa kwa siku mbili mfululizo katika ukumbi huohuo.
Picha chini ni baadhi ya taswira za washiriki wa filamu hiyo.
No comments:
Post a Comment