Mwananchi aliyetembelea Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), akipewa maelezo na Afisa Habari Mkuu wa Mamlaka hiyo, Rose Mdami (kulia) kuhusu taarifa mbalimbali zinazoandaliwa na Mamlaka hiyo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Polisi nchini, Tumaini Julius, akitoa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi hilo, katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jjijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akipiga picha na sanamu la askari linaloonyesha mavazi yaliyokuwa yanavaliwa na askari wa kike, katika maonesho hayo ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanaendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi
Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji, Dickson Rweza (kushoto), akitoa maelezo kwa
mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika
maonesho hayo ya Wiki ya Utumishi wa Umma
yanaendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. (Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment