Balozi Seif Ali Iddi akiufunga Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi kwenye ukumbi wa Braza hilo hapo Mbweni uliokuwa ukijadili Bajeti nya Serikali kwa mwaka 2015/2016.
Balozi Seif Ali Iddi akiufunga Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi kwenye ukumbi wa Braza hilo hapo Mbweni uliokuwa ukijadili Bajeti nya Serikali kwa mwaka 2015/2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed akitoa shukrani kwa nmiaba ya Mawaziri wenzake kwenye hitimisho la Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mwakilishi wa Viti Maalum Wanawake CCM Mh. Panya Ali Abdulla akitoa shukrani kwa niaba ya Wawakilishi wenzake (Back Banchers) wakati wa hitimisho la Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mtangazaji wa Shrika la Utangazaji Zanzibar Khamis Fakih Moh’d akipata
ufafanuzi kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada
ya kuufunga Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi mapema asubuhi. Mwanzo
kutoka kulia ni Repota wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC - TV), Hadia
Kombo.
Na Othman Khamis Ame
Ofisiya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
26/6/2015.
MAKAMU wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati harakati za uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2015 zimeanza kwa vyama vya siasa kutafuta wagombea wa nafasi
mbali mbali za uongozi Viongozi pamoja na wananchi wanaweza kuchaguana bila ya
kutukanana,kugombana nakuepuka kuhamasishana katika kufanya vurugu zinazoweza
kuvuruga zoaezi zima la uchaguzi huo.
Alisema
mafanikio yaliyopatikana kwa muda mrefu yanategemea kudumu kwa hali ya amani na
utulivu kwa vile kila mwana jamii na mwananchi ana haki na wajibu wa kusimamia
maendeleo hayo.
Akiufunga
Mkutano wa 20 wa Baraza la Wawakilishi uliokuwa ukijadili Bajeti ya Serikali ya
mwaka 2015/2016 katika ukumbi wa Baraza hilo Mbweni nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar Balozi Seif alielezea matumaini yake kwamba wananchi wataendelea kuiamini na kuiunga
mkono Serikali yao inayoongozwa na Rais kutoka CCM.
Alitanabahisha kwamba Serikali itahakikisha ulinzi na usalama unaimarika
na haitokuwa tayari kumvumilia mtu au kikundi chochote kitakachovunja
sheria na kuihatarisha amani na utulivu
wa nchi.
Balozi Seif Ali Iddi alionya kwamba watu wasifikirie hata siku moja
kwamba vikundi vinavyojitayarisha au kutayarishwa na wachochezi kufanya vitendo vya kuhatarisha
amani ya nchi vinaikomoa Serikali, bali vielewe kwamba vinajikomoa vyenyewe.
Akizungumza bila
ya uwepo wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama cha Wananachi (CUF)
ndani ya kikao hicho Balozi Seif aliwaeleza wananchi kwamba yapo mafanikio makubwa
yaliyopatikana ndani ya Kipindi cha
Kwanza cha Awamu ya Saba katika Sekta mbali mbali ikiwemo Afya, Elimu, Utalii,
Maji, Miundombinu na Mawasiliano, Sekta za Uzalishaji viwandani, kilimo, mifugo
na uvuvi.
Alisema mafanikio hayo ya kupigiwa mfano yametokana
na utekelezaji sahihi wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010 – 2015 chini ya usimamizi wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Makamu
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mheshimiwa
Dkt. Ali Mohamed Shein ambapo hakuna shaka
kwa mafanikio hayo.
Wananchi walio wengi watamrejesha tena
kuiongoza Zanzibar iliyoamua kuwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa.
Balozi Seif alisema katika kipindi cha miaka mitano (2010 – 2015),
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa fidia ya jumla ya Shs. 7,129,591,148
za kuendeleza kilimo, kwa ajili ya ununuzi wa mbolea, madawa, mbegu na kutoa
huduma za matrekta kwa wakulima.
Alisema hadi kufikia asilimia 5.6 mwaka 2014 hali inayotokana na
kuongezeka kwa uzalishaji wa ndani
unaotokana na juhudi zilizochukuliwa na Serikali katika kuwapatia ruzuku
za pembejeo wakulima hapa Nchini.
Balozi Seif alieleza kwamba Kilimo bado kinaendelea kuwa muhimili Mkuu wa
Uchumi wa Taifa kwa kutoa ajira kwa wananchi walio wengi na ndio maana Serikali
ikalazimika kutekeleza mipango na miradi mbali mbali ya kilimo.
Akigusia sekta ya utalii inayoendelea kuimarika na kuwa tegemeo la
kuongeza pato la Taifa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema idadi ya watalii walioingia Nchini
imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia watalii Laki 274,619 mwaka
215.
Alisema ongezeko hilo linatokana na kuimarika kwa miundombinu ya utalii pamoja na hali ya kudumisha amani na
amewahakikishia watalii usalama wao kwa kipindi chote ambnacho watakuweo hapa
Nchini.
Alifahamisha kwamba katika kuimarisha zaidi sekta ya Utalii Serikali
imeamua kuibadilisha mandhari ya Hoteli ya Bwawani ambayo ina Historia kubwa
baada ya kuatikana kwa mwekezaji ambae yuko tayari kuibadilisha hali hiyo.
Balozi Seif alisema Mazungumzo baina ya Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar
na Mwekezaji aliyechaguliwa kuendesha mradi huo yamefikia hatua nzuri na
kinachobakia kwa sasa ni Serikali kumkabidhi mradi huo mwekezji husika na
kufungaq naye mkataba.
Kuhusu Sekta ya miundombinu ya
mawasiliano ya Bara bara Mtendaji Mkuu huyo wa Serikali alisema Serikali
imejenga bara bara mpya kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita mia 243.85
na Bara bara nyengine zenye urefu wa kilomita 39.3 zimejengwa kwa kiwango cha
kifusi na zile zenye urefu wa Kilomita 656 zimefanyiwa matengenezo mbali mbali.
Alisema miundombinu hiyo kwa kiasi kikubwa itasaidia kuimarisha uchumi wa Taifa na kutoa wito kwa
wananchi pamoja na watumiaji wa bara bara hizo kuzitunza kwa faida yao na
vizazi vijavyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaasa wale watu wenye tabia ya
kuzichoma bara bara hizo kwa makusudi kutokana na ushabiki wa kisiasa ni vyema
wakaacha tabia hiyo yenye kuigharimu fedha nyingi Serikali Kuu katika
kuzitengeneza upya.
Balozi Seif aliwashukuru na kuwapongeza Wajumbe wote wa Baraza la
Wawakilishi kwa michango,mapendekezo na ushauri walioutoa wakati wa kuzijadili
Hotuba za Bajeti zilizowasilishwa kwenye Baraza hilo la WEawakilishi Zanzibar.
Alisema katika Mikutano yote ya Baraza la Wawakilishi, Mkutano wa mwaka
huu ulikuwa wa kupigiwa mfano kwa kupitishwa bajeti zote kwa urahisi na bila ya
pingamizi zozote.
Balozi Seif alieleza kwamba upitishwaji wa Bajeti hizo ulikuwa rahisi
kutokana na sababu ya kutumia mfumo mpya wa Bajeti uitwao Program Based Bujet {
PBB } uliosaidia kupunguza vikwazo kutoka kwa Wajumbe wakati wa Kamati.
Baraza hilo la Wawakilishi la Nane tokea kuasisiwa kwake hadi sasa
limeshafanya jumla ya Mikutano 20 katyika Mikutano ambayo jumla ya maswali ya
msingi 1,630 na yale ya nyongeza elfu 3,277 yameulizwa kwa Serikali na
kujibiwa.
Baraza hilo pia limefanikiwa kujadili na kupitisha miswada ya sheria
ipatayo 63 na hatimae kutungwa kwa sheria kutokana na miswada hiyo pamoja na
kuidhinisha Bajeti ya Serikali na Mawizara mara Tano hadi kipindi hichi Bajeti
ambazo zimesaidia kufanikisha kupatikana kwa maendeleo makubwa hapa Nchini.
No comments:
Post a Comment