TANGAZO


Tuesday, June 2, 2015

Alshabaab ladaiwa kuviteka vijiji Kenya


Alshabaab

Hofu kubwa imetanda Kaskazini mwa nchi ya Kenya,baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba kundi la wapiganaji wa Al shabaab Limeviteka vijiji kadhaa katika mpaka wa Kenya na somalia.
Mamia ya wakaazi wameyatoroka makaazi yao kufuatia taarifa za kuwepo kwa wapiganaji wa Alshabaab wapatao thelathini.
Shule nne zinaripotiwa kufungwa.
Naibu kamishna wa kaunti ya Mandera amenukuliwa akisema kwamba wamepokea ripoti za kuwepo kwa wapiganaji hao na watawaandama na kulidhibiti eneo hilo.

No comments:

Post a Comment