Maelfu ya watalii wanaondoka Tunisia baada ya shambulio katika hoteli ya watalii iliyosababisha vifo vya watu 38 wengi wao wazungu.
Makampuni ya utalii pia yanavunja safari za kwenda huko.
Katika uwanja wa ndege wa Hammamet, karibu na Tunis, watalii wamepanga foleni kusubiri kuondoka nchini humo.
Serikali ya Tunisia inasema kuwa ulinzi umezidishwa katika maeneo ya utalii huku wanajeshi wa akiba wakitakiwa kuripoti kazini mara moja.
Aidha serikali imetangaza kuwa itafunga misikiti 80, inayodaiwa kuwa inafundisha utumizi wa nguvu na Jihad.
Islamic State imesema imehusika na shambulio hilo.
Mshambuliaji aliyekuwa na bunduki, baadae alipigwa risasi na kuuawa.
Wakati huo huo inaaminika sasa kuwa 15 kati ya wale waliouawa huko Tunisia ni raia wa Uingereza.
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, amesema shambulio hilo ni kumbusho la kikatili na kusitikisha, kwamba kuna tisho la ugaidi dunia nzima
"Nitahakikisha, tunafanya tuwezalo kusaidia, na kuwakinga watu na mashambulio ya kigaidi''.
''Tunawakumbuka na kuwaombea waliofiwa, na wale waliojeruhiwa''.
''Tunashirikiana na wakuu wa Tunisia, kujua idadi kamili ya Waingereza waliouliwa.''
Lakini wananchi wa Uingereza wanafaa kujitayarisha, kuwa wengi waliouwawa ni Wangereza."Alisema Cameroon.
No comments:
Post a Comment