TANGAZO


Wednesday, May 13, 2015

Shule ya Sekondari Mtakuja ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam yapokea msaada wa kompyuta toka Vodacom Foundation

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi beach jijini Dar es Salaam,wakishusha vifaa vya kompyuta mpakato kwa kushirikiana na maofisa wa Vodacom Tanzania,Jumla ya kompyuta(25) pamoja na  vifaa vingine vimetole msaada na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung na vitafungwa hivi karibuni kwa ajili ya kufundishia somo la kompyuta shuleni hapo. 
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza  akiwapa  maelezo wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam juu ya utumiaji wa kifaa maalumu cha kuhifadhia na  kuchajia kompyuta mpakato. Jumla ya kompyuta(25) pamoja na  vifaa vingine vimetole msaada na mfuko huo kwa kushirikiana na Samsung na vinategema kufungwa kwa ajili ya kufundishia somo la kompyuta shuleni hapo. 
Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika shule ya sekondari ya Mtakuja ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, Elizabeth Claud  akibofya komputa mpakato wakati Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza alipokuwa akiwaonyesha kompyuta hizo. Jumla ya kompyuta(25) pamoja na  vifaa vingine vimetole msaada na mfuko huo  kwa kushirikiana na Samsung na vinategema kufungwa hivi karibuni kwa ajili ya kufundishia somo la kompyuta shuleni hapo. 
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza,akifurahia jambo pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Beach jijini Dar es Salaa, wakati alipokuwa akiwaonyesha  moja ya Kompyuta mpakato  kati ya 25  pamoja na  vifaa vingine vilivyotole msaada na mfuko huo kwa kushirikiana Samsung.Kompyuta hizo zinategemea kufungwa  hivi karibuni kwa ajili ya kufundishia somo la kompyuta shuleni hapo. 
Kompyuta mpakato 25 zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation  kwa ushirikiano na Kampuni ya Samsung katika shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam zikiwa zimehifadhiwa katika kifaa maalumu cha kuhifadhia na kuchajia Kompyuta hizo.

No comments:

Post a Comment