TANGAZO


Friday, May 8, 2015

Pele afanyiwa upasuaji

Pele
Aliyekuwa nyota wa timu ya taifa ya Brazil Pele amefanyiwa upasuaji wa kibofu cha mkojo katika hospitali moja mjini Sao Paulo.
Vyombo vya habari nchini Brazil vimeripoti kwamba anaendelea vyema.
Pele wakati alipokuwa akiichezea timu ya taifa ya Brazil
Pele mwenye umri wa miaka 74 alilazwa katika hospitali hiyo takriban miezi sita iliopita kwa upasuaji wa dharura ili kuondoa mawe katika figo yake.
Pele ambaye jina lake ni Edson Arantes do Nascimento alifunga zaidi ya mabao 1200 wakati alipokuwa akicheza soka na kuisaidia Brazil kushinda mataji matatu ya kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment