TANGAZO


Friday, May 1, 2015

Nepal:Waathiriwa wasema hawajapata msaada


Wana vijiji wa Kathmandu

Wana viijiji walio karibu na kitovu cha tetemeko la arthi nchini Nepal wamesema hawajapokea msaada wowote wiki moja baada ya kutokea mkasa huo.
Wakaazi katika kijiji kimoja wameelezea jinsi wanavyopata mchele kwa mkopo kutoka vijiji jirani.
Mwandishi mmoja aliyefika eneo hilo amesema kila kitu kimeharibiwa na tetemeko hilo ikiwemo makaazi na barabara.
Pia alishuhudia uharibifu sawa katika maeneo ya karibu.
Serikali ya Nepal imeomba msaada wa Helikopta kutoka kwa serikali za nje kuwasilisha misaada maeneo ya milima.
Zaidi ya watu elfu sita walifariki dunia kutokana na tetemeko hilo la arthi.

No comments:

Post a Comment