Mnamo 13 mwezi May jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.
20.00pm-Onyo Burundi
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameonya kuwa atalipiza kisasi dhidi ya mtu yeyote ambaye atashambulia Burundi.''katika taarifa yake amesema kuwa ''hatutakubali mtu yeyote kuwasha moto Burundi''.
18.00-makaribisho ya Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametuma ujumbe katika mtandao wake wa tweetter kwa lugha ya kirundi akisema kuwa ''Nilifurahi kuona vile raia wa Burundi walivyonipokea katika mji wa Bujumbura pamoja na mikoa mingine
17.45pm-Hofu yatanda Burundi
Kuna mazingira ya hofu na switofahamu katika mji wa Bujumbura kufuatia kufeli kwa jaribo la mapinduzi kulingana na mkaazi mmoja wa mji huo.Serge Ntabikiyoboka anasema kuwa hadhani kwamba taifa hilo literejea katika hali yake ya kawaida hivi karibuni.
17.30-UN ina wasiwasi kuhusu Burundi.
Tume ya haki za binaadamu katika umoja wa mataifa imeonya kuhusu ulipizaji kisasi kufuatia jaribio la mapinduzi nchini Burundi.Msemaji wake Rupert Coleville amesema kuwa tume hiyo ina wasiwasi kuhusu matukio ya taifa hilo katika kipindi cha siku mbili zilizopita.
16.20pm-Nurunziza awasili Bujumbura
Rais Pierre Nkurunziza amewasili katika makao ya rais mjini Bujumbura kupitia msafara mkubwa wa magari .Alikaribishwa na umati mkubwa wa wanachama wa chama chake ambao walikuwa wamevaa mavazi ya bendera za chama hicho huku wakicheza densi.
16.10pm-wafuasi wa Nkurunziza
Mwandishi wa BBC Ruth Nesoba ametuma picha za wafuasi wa rais Pierre Nkurunziza kufuatia kuwasili kwa rais huyo katika ,mji mkuu wa Bujumbura
16.00pm-wanajeshi walioasi
Baadhi ya picha za wanajeshi waasi waliohusika na jaribio la mapinduzi nchini Burundi ambao wamekamatwa
13.30-Raia wamlaki rais Ngozi
Mashahidi wameiambia BBC kwamba rais Pierre Nkurunziza amerudi kwao huko Ngozi nchini Burundi na amekuwa akiendeshwa katika gari lilo wazi upande wa juu na kwamba raia wamemlaki kwa shangwe na vigelegele
13.23pm-Nkurunziza arudi nyumbani kwake Ngozi
Shirika la habari la AFP limeripoti kwamba rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amerudi nyumbano kwao huko Ngozi yapata kilomita 140 kazkazini mwa mji mkuu wa Bujumbura kulingana na duru ambazo hazikutaka kujulikana zilizo karibu na kiongozi huyo.''Aliwasili katika eneo la Ngozi siku ya Alhamisi.Ni hapa ambapo anatarajiwa kulihutubia taifa kuhusu jaribio la mapinduzi lililofeli'',.AFP lilimnukuu aliyetoa habari hizo.
12.00-Raia watakiwa kuendeleza maandamano
Kiongozi wa kundi la kiraia linalopinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu amewataka raia nchini humo kuendelea na maandamano kulingana na shirika la habari la AFP.
Vital Nshimiriman amesema kuwa licha ya kundi hilo kupinga jaribio hilo la mapinduzi,vile raia walivyowashangilia wanajeshi wa jaribio hilo kulionyesha kwamba kuna hamu kubwa ya mabadiliko.
10.30am-Majenerali waasi kushtakiwa
Nukuu muhimu kutoka kwa Gervais Abayeho,msemaji wa rais Pierre Nkurunziza akizungumza na kipindi cha BBC cha Newsday.''Mapinduzi hushirikisha watu wengi Kuna wanajeshi wa nyadhfa za chini ambao wamesalimu amri na ambao wanawasaidia maafisa wa poisi na uchunguzi wao,lakini ninaamini watu waliopanga mapinduzi hayo ,wale viongozi hilo ni swala jingine ni lazima washtakiwe.hakuna mgawanyiko katika jeshi.Iwapo unaweza kuwaangalia wale waliokuwa wakipanga kutekeleza mapinduzi ni wachache ...kundi dogo la jeshi'',alisema..
10.00am-Majenerali waasi wakamatwa:
Majenerali wawili waliotekeleza jaribio la mapinduzi nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza wamekamatwa.
Hatahivyo kiongozi wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare ametoroka na anasakwa kulingana na msemaji wa rais.
Awali Jenerali Niyombare alikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na wafuasi wake watajisalimisha akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuwa amerudi nchini Burund na kwamba anatarajiwa kulihutubia taifa.
No comments:
Post a Comment