Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akifafanua jambo linalohusu kero ya Muungano kikao kilichofanyika mjini Dar es salaam kati yake na viongozi wa Hazina siku moja kabla ya kwenda Zanzibar.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akisalimiana na Mhe. Omar Y. Mzee Waziri wa Fedha Zanzibar mara baada ya kuwasili Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo kuhusu kutatua kero za Muungano hapa Zanzibar.
Waziri wa Fedha Zanzibar, Mhe. Omar Y. Mzee Waziri akisisitiza jambo kwa ujumbe kutoka SMT na SMZ katika kikao cha kutatua kero za Muungano kilichofanyika leo mjini Zanzibar. Kutoka kushoto kwa SMZ ni Bw. Mwita Mgeni Kamishna wa Bajeti – Wizara ya Fedha ZNZ, Bw.Abdi Fakih Kamishna- ZRB, Mhe. Omar Y. Mzee Waziri wa Fedha – ZNZ na Bw. Juma Ameir , Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha- ZNZ.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akionyesha kwa wajumbe kutoka SMT na SMZ mfano wa kero ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi mara moja katika kikao maalum kilichofanyika Zanzibar kwa madhumuni ya kutatua kero hizo.
Prof. Adolf Mkenda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha akijaribu kutetea hoja yake kwa Waziri wa Fedha Zanzibar, Mhe. Omar Y. Mzee ( hayupo kwenye picha)katika kikao cha kutatua kero za Muungano kilichofanyika leo hapa Zanzibar. (Picha zote na Ingiahedi Mduma na Scola Malinga – Zanzibar)
No comments:
Post a Comment