Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa limeliokoa kundi la kwanza la takriban wasichana 300 na wanawake waliookolewa kutoka kwa kundi la Boko Haram kwenye kambi moja ya wakimbizi.
Watu hao wanaripotiwa kusafiri kwa siku tatu kutoka msitu wa Sambisa ulio kaskazini mashariki mwa nchi.
Karibu watu 700 wanaripotiwa kuokolewa wiki hii wakati jeshi linapoendelea na operesheni ya kulitimua boko haram kutoka kwa ngome zao za mwisho.
Hatma ya wasichana wengine 200 waliotekwa kutoka mji wa Chibok mwaka mmoja uliopita bado haijulikani.
No comments:
Post a Comment