TANGAZO


Friday, May 15, 2015

EPL kuendelea wikiendi hii

Viwanja saba kuwaka moto wikiendi hii
Ligi ya England itaendelea tena wikiendi hii kwa nyasi za viwanja saba kuwaka moto katika siku ya jumamosi .
Southampton walioko katika nafasi ya 7 huku wakiwa wamejikusanyia alama 57 watakua wenyeji wa Aston Villa mchezo utakaofanyika katika uwanja wa St Mary's.
Mechi za ligi ya Uingereza
Burnley ambao tayari wameshuka daraja watakua katika uwanja wao wa nyumbani Turf Moor kuwakabili Stoke City.
Katika dimba la Loftus Road QPR watakua na kibarua cha kuwakabili Newcastle huku QPR wakikamilisha ratiba baada ya kuwa wameshashuka daraja tayari.
Sunderland atakua nyumbani Brittania kuwaalika Leicester City huku kila timu ikihitaji alama tatu kuweza kujinasua na janga la kushuka daraja.
Mechi za ligi ya Uingereza
Tottenham ambao wamepoteza nafasi ya kucheza michuno klabu bigwa ulaya watakua wanasaka tiketi ya kucheza Europa Ligi watakapo wakabili Hull City.
West Ham walioko nafasi ya 10 watakua katika dimba lao la Upton Park, kupepetana na Everton.Huku Majogoo wa jiji Liverpool wakiwakabili Tai wa Crystal Palace.
Kompany
Ligi hii itaendelea tena jumapili kwa michezo miwili kwa Swansea kucheza Man City huku Manchester United wakionyeshana ubavu na Arse.

No comments:

Post a Comment