Mwenyekiti wa Madereva Tanzania Clement Masanja, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwajulisha madereva wote nchini kuwa mwaka huu wamekubaliana na Mamlaka husika kuwa hakutakuwa na mafunzo kama ilivyoelezwa hapo awali. Kulia ni Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.(Picha zote na Idara ya Habari, Maelezo, Dar es Salaam)
Na Pius Yalula-Maelezo-Dar es Salaam
13.5.2015
SERIKALI imesema hakutakuwa na mafunzo kwa madereva wa malori na mabasi
na wala hawatakiwi kwenda kusoma kozi fupi ili kuhuisha leseni zao kama ilivyokuwa
imetangazwa hapo awali na kusababisha
mgomo.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani
Mohamed Mpinga wakati akitoa tamko hilo kwa waandishi wa habari leo mjini Dar
es Salaam.
Alisema kuwa madereva wenye daraja E, C, C1, C2 na C3 walitakiwa kupata
mafunzo ya muda mfupi kila baada ya miaka 3 kulingana na kanuni ziliandaliwa
mwaka 2014 kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA), Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), Chuo cha
Taifa ya Usafishaji(NIT), Vyama vya Madereva, Ofisi ya Mwanasheri Mkuu wa
Serikali na Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo Tanzania (TATOA) , lakini kwa mwaka huu hawatatekeleza
kanuni hiyo.
Kamanda Mpinga alisisitiza kuwa kanuni hiyo
hatatumika mwaka huu badala yake madereva wataendelea na utaratibu wao wa
zamani wa kubadilisha na kuhuisha leseni zao kwa zile ambazo zitakuwa
zimekwisha bila kuulizwa vyeti.
Aliongeza kuwa hadi hivi sasa mitala ya
mafunzo hayo ya muda mfupi bado haijakamilika na wala Serikali haijawahi
kupanga ada za mafunzo hayo , kwa hiyo utaratibu wa zamani utaendelea kutumika
kama ulivyokuwa hapo awali.
Kamanda Mpinga alitoa wito kwa madereva wote
kuwa wavumilivu kwa matatizo yao wakati Kamati ya kudumu ya kutatua matatizo ya
sekta ya usafishaji ikendelea kuyatafutia ufumbuzi.
Katika hatua nyingine Kamanda huyo ametoa
wito kwa wananchi na wasafiri kutoa taarifa kwa viongozi wa Jeshi hilo endapo
wanaona Askari wao au dereva anatenda
vitendo visivyo vya kimaadili ili aweze kuchukuliwa hatua.
Alisema kuwa jeshi la Polisi kikosi cha
usalama barabarani kipo wakati tayari kupokea malalamiko ya kuyachukulia hatua
ili kulinda maisha ya wasafiri na mali zao, hivyo ni vizuri wakaripoti wale
wote wanaohatarisha maisha ya wenzao.
No comments:
Post a Comment