TANGAZO


Wednesday, April 8, 2015

Yanga yaikung'uta Coastal Union ya Tanga mabao 8-0 Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo dhidi ya Coastal union ya Tanga wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.  Katika mchezo huo, Yanga imeifunga Coastal Union mabao 8-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Amis Tambwe wa Yanga, akiwa na baadhi ya wachezaji wenzake wakishangilia moja ya mabao aliyoifungia timu yake hiyo, wakati wa mchezo huo leo jioni, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. 
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la 5 la timu hiyo wakati wa mchezo huo. 
 Ubao wa matangazo ukionesha Yanga mabao 5, Coastal Union 0.
Amis Tambwe wa Yanga akiwa na mpira akiwatoka wachezaji wa Coastal Union. 
Mtama Bakari wa Coastal Union akimkwatua Haruna Niyonzima wa Yanga. 
Haruna Niyonzima wa Yanga (8), akijaribu kuruka kiunzi cha Shekuwe Mohamed wa Coastal Union. 
 Kpah Sherman wa Yanga, akimtoka Shekuwe Mohamed wa Coastal Union. 
  Kpah Sherman wa Yanga, akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Mtama Bakari wa Coastal Union. 
 Kpah Sherman wa Yanga, akipambana na Mtama Bakari wa Coastal Union kuwania mpira wakatiwa mchezo huo.
 Nizar Khalfan wa Yanga akiwania mpira na Chuma Yussuf wa Coastal Union.
Golikipa Bakari Fikirini wa Coastal Union akiudaka mpira uliokuwa umepigwa na Simon Msuva (wa pili kulia) wa Yanga. 
 Amis Tambwe wa Yanga akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Abdulhalim Humud wa Coastal Union.
Mtama Bakari wa Coastal union akiuondoa mpira miguuni mwa Amisi Tambwe wa Yanga. 
 Haruna Niyonzima wa Yanga akikimbilia mpira na Mtama Bakari wa Coastal Union.
Edward Charles wa Yanga, akijaribu kumhadaa Mtama Bakari wa Coastal Union. 
 Edward Charles wa Yanga, akimtoka Mtama Bakari wa Coastal Union. 
 Mtama Bakari akiuondoa mpira miguuni mwa Edward Charles wa Yanga.
 Simon Msuva akishangilia moja ya mabao aliyoifungia timu yake ya Yanga katika mchezo huo.
 Ubao wa matangazo ukionesha Yanga mabao 7, Coastal union 0.
Simon Msuva akimpiga chenga Juma Mtenje wa Coastal Union. 
Amis Tambwe (kulia) na Haruna Niyonzima (anaye sali), wote wa Yanga, wakishangilia bao la 8, aliloifungia timu yake hiyo dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga ilishinda mabao 8-0. 
Amis Tambwe (kulia) na Haruna Niyonzima wote wa Yanga, wakishangilia bao la 8, aliloifungia timu yake hiyo dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga ilishinda mabao 8-0. 
Hapa ikiwa ndio mwisho wa mchezo huo, ubao wa matangazo ukionesha Yanga mabao 8 na Coastal Union 0. 
Amisi Tambwe akikabidhiwa mpira na mwamuzi wa mchezo huo, Simon Mbelwa baada ya kuifungia timu yake ya Yanga mabao 3 katika mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga wakipagawa kwa furaha baada ya timu yao kushinda kwa mabao 8-0.

No comments:

Post a Comment