Wachezaji wa Bercelona Legends, wakiwa na baadhi ya watu wenye ualbino, kwenye mstari wakisubiri kukaguliwa na mgeni rasimi, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara. akisalimiana na wachezaji wa Bercelona Legends na baadhi ya watu wenye ualbino.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akizungumza na mtoto mwenye ualibino, aliyebebwa na Patrick Kluivet wa Bercelona Legends.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara. akisalimiana na wachezaji wa Tanzania Legends.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meki Sadiki (kulia kwake), akipiga picha kwenye bango la kupiga vita mauaji ya albino akiwa pamoja na wachezaji wa Bercelona Legends.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akipiga picha ya pamoja na wachezaji wa Tanzania na Bercelona Legends kabla ya mpambano wao, uwanjani hapo.
Waamuzi wa mchezo wa maveterani wa Tanzania na Bercelona wakipiga picha ya pamoja kabla ya mchezo huo leo.
Kikosi cha wachezaji wa Tanzania Legends, kikipiga picha ya pamoja kabla ya mchezo na wenzao wa Bercelona, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Kikosi cha Bercelona Legends, kikipiga picha ya pamoja kabla ya mchezo na wenzao wa Tanzania Legends, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Patrick Kluivert wa Bercelona Legends, akielekea uwanjani kwa ajili ya mchezo dhidi ya Tanzania Legends, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Patrick Kluivert na wenzake wa Bercelona Legends, akiwa amembeba mtoto Sharifa, mwenye ualbino wakiingia Uwanjani kabla ya mchezo na timu ya Tanzania Legends, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Patrick Kluivert wa Bercelona Legends, akiwa amembeba mtoto Sharifa, mwenye ualbino kabla ya mchezo na timu ya Tanzania Legends, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Kushoto ni mchezaji mwenzake, Luis Garcia.
Patrick Kluivert na wenzake wa Bercelona Legends, akiwa amembeba mtoto Sharifa, mwenye ualbino wakiingia Uwanjani kabla ya mchezo na timu ya Tanzania Legends, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Patrick Kluivert (mbele) na Luis Garcia wa Bercelona Legends, wakisalimiana na wachezaji ya Tanzania Legends, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo, kabla ya kuanza mchezo kati yao jijini Dar es Salaam leo.
Patrick Kluivert (mbele) na wenzake wa Bercelona Legends, wakisalimiana na wachezaji ya Tanzania Legends, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo, kabla ya kuanza mchezo kati yao jijini Dar es Salaam leo.
Mustafa Hoza wa Tanzania Legends akikimbilia mpira na Luis Garcia wa Bercelona Legends, wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mustafa Hoza wa Tanzania Legends akipambana na Luis Garcia wa Bercelona Legends, wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Haruna Moshi wa Tanzania Legends akiwania mpira na Mendieta wa Bercelona Legends.
Yussuf Macho (kushoto), akishangilia na mchezaji mwenzake, Aboubakar Kombo, bao aliloisawazishia timu yao ya Veterani ya Tanzania dhidi ya wenzao wa Bercelona, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Hadi nusu ya kwanza ya mchezo huo, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Yussuf Macho (kushoto), akishangilia na mchezaji mwenzake, Aboubakar Kombo, bao aliloisawazishia timu yao ya Veterani ya Tanzania dhidi ya wenzao wa Bercelona, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Hadi nusu ya kwanza ya mchezo huo, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Wachezaji wa timu ya Veterani ya Tanzania wakishangilia bao la kusawazisha lililofungwa na Yussuf Macho, wakati timu hiyo ilipopambana na veterani wa Barcelona, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mpaka mapunziko timu hizo zilikuwa zimeshafungana bao 1-1, huku Tanzania Legends wakisawazisha bao kupitia kwa mchezaji wao Yussuf Macho 'Musso'. Hadi mwisho mpira ulipomalizika Bercelona Legends waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

No comments:
Post a Comment