Pages

Saturday, April 25, 2015

Simba yaipiga Ndanda FC mabao 3-0 Ligi Kuu ya Vodacom Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Awadh Juma (kulia) wa Simba akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Kassian Ponera wa Ndanda FC wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilishinda kwa mabao 3-0. (Picha zote na Khamisi Mussa)
Emmanuel Okwi wa Simba akimtoka Azizi Sibo wa Ndanda FC wakati wa mchezo huo.
Kocha wa Simba, Goran Kopunovic akiwaelekeza wachezaji wake jinsi ya kukabiliana na wachezaji wa Ndanda FC wakati wa mchezo huo. 
Wachezaji wa Ndanda FC, wakimlalamikia mwamuzi wa mchezo huo, Livingston Liza.
Mchezaji Ramadhan Singano wa Simba, akishangilia bao lake kwa kusujudu kwenye kibendera cha kona wakati timu hiyo ilipopambana na Ndanda FC katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa  Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 3-0. 
Mchezaji Ramadhan Singano (aliyeshikwa mabega) wa Simba, akinyanyuliwa huku mwamuzi Livingston Liza akiwataka kurudi uwanjani, wakati alipokuwa akishangilia bao lake kwa kusujudu kwenye kibendera cha kona, wakati timu hiyo ilipopambana na Ndanda FC katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa  Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa Simba wakipongezana baada Mkude kuifungia timu yake bao la kwanza dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa  Dar es Salaam leo. 
Wachezaji wa Simba wakipongezana baada Mkude kuifungia timu yake bao la pili dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa  Dar es Salaam leo. 
Mashabiki wa Simba, wakishangilia moja ya mabao 3 ya timu hiyo dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa  Dar es Salaam leo.
Ramadhan Singano 'Messi' akijaribu kumpiga chenga Azizi Sibo wa Ndanda FC.
Ramadhan Singano 'Messi' akiwania mpira uliokuwa ukidhibitiwa na Shukuru Chachala wa Ndanda FC.
Ramadhan Singano 'Messi' akikwatuliwa na Shukuru Chachala wa Ndanda FC, wakati wa mchezo huo..
Mashabiki wa Ndanda FC, wakiishangilia timu yao wakati wa mchezo huo dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 3-0.

No comments:

Post a Comment