Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi mshindi wa simu ya kisasa aina ya Solar 5, Richard John, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam mara baada ya kuibuka mshindi wa droo hiyo ya tatu ya kujishindia pikipiki na simu ya mwezi wa Aprili inayoendeshwa na kampuni hiyo. Katikati akishuhudia ni Bw. Gideon Fumbuka ambaye naye alijinyakulia simu kisasa aina ya P40. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
Mshindi wa droo ya bahati nasibu ya kujishindia
pikipiki inayoendeshwa mwezi huu wa Aprili na StarTimes Tanzania, Mary Luis
Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama,
jijini Dar es Salaam akionyesha nyaraka
za pikipiki kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa
katika ofisi za kampuni jijini Dar es Salaam. Pamoja naye katika makabidhiano
ni Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif, kujiunga
na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia
shilingi 10,000/- na kuendelea.
Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi nyaraka za pikipiki mshindi wa droo ya tatu ya kujishindia pikipiki ya mwezi wa Aprili, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama, jijini Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
Namba ya smartkadi ya king’amuzi cha mshindi wa
nne wa droo ya pikipiki ya mwezi Aprili inayoendeshwa na StarTimes ikionekana
katika luninga mara baada ya kuchezeshwa kwa droo ya bahati nasibu mbele ya
waandishi wa habari. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes
wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
Na Dotto Mwaibale
MKAZI wa Kijitonyama Dar es Salaam, Mary Luis Tumsifu (40) ambaye anajishughulisha na biashara ya kuuza vyakula vya mifugo na ufugaji amekabidhiwa zawadi ya pikipiki baada ya kuibuka mshindi katika droo ya tatu ya mwezi ya bahati nasibu inayoendeshwa na StarTimes Tanzania.
MKAZI wa Kijitonyama Dar es Salaam, Mary Luis Tumsifu (40) ambaye anajishughulisha na biashara ya kuuza vyakula vya mifugo na ufugaji amekabidhiwa zawadi ya pikipiki baada ya kuibuka mshindi katika droo ya tatu ya mwezi ya bahati nasibu inayoendeshwa na StarTimes Tanzania.
Akizungumza
wakati anakabidhiwa pikipiki yake Tumsifu amebainisha kuwa amefurahia sana
zawadi hiyo kwani hakutegemea kama angeweza kushinda kwani alilipia kutazama
vipindi anavyovipendelea.
“Sikutarajia
kama nitajishindia pikipiki lakini tayari ndiyo bahati imekwishaniangukia mimi.
Ni kweli nilikuwa nafahamu kuhusu bahati nasibu hii kupitia njia mbalimbali
kama vile kutumiwa ujumbe mfupi pamoja na matangazo.
Kwa kawaida huwa nalipia
kifurushi kile kikubwa cha shilingi 30,000/- cha Kili. Mimi ni mpenzi sana wa ‘Series’
na mwanangu anapenda kuangalia chaneli ya watoto ya ‘Nickelodeon’. Hivyo huwa
sina budi kulipia ili mimi na mwanangu tufarahie vipindi tunavyovipenda.”
Alisema Tumsifu
“Mimi
ni mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo lakini pia ni mfugaji. Kusema kweli hii
zawadi imekuja kipindi ambacho sijaitarajia hivyo nashindwa hata kuelezea
nitaitumia kwa namna gani. Naweza kuifanya kama biashara au mimi mwenyewe
nikajifunza na kuwa dereva bodaboda.”
Alisema kwa masihara huku akicheka.
Akizungumzia
kuhusiana na imani waliyonayo wateja juu ya bahati nasibu hii kuwa ni uzushi, Tumsifu alifafanua kuwa, “Kwanza kabisa ningependa kuwatoa hofu na
kuwahakikishia wateja na watanzania kuwa kitu kama hicho hakipo.
Kwa mfano mimi
sifahamiani na mtu yeyote StarTimes, huwa nalipia vifurushi vya mwezi kama
wateja wengine lakini nimebahatika nimeshinda. Hivyo basi nawaomba wengine pia
waondoe mawazo hayo na kushiriki pindi wanapoambiwa wafanye hivyo.”
“Nashukuru
sana kwa zawadi hii, ninaahidi nitaitumia vema ili inisaidie katika shughuli
zangu. Wito wangu, kwanza kabisa kwa StarTimes, nawapongeza kwa huduma bora
wanazotupatia wateja wao tena kwa bei nafuu, ninawaomba wazidi kuboresha zaidi,
wasikilize maoni yetu ili tuzidi kufurahia.” Alihitimisha. Tumsifu
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif
aliwataka wateja wa kampuni hiyo kuchangamkia hii fursa kwa kujiunga zaidi na
vifurushi ili waweze kuburudika na pia kushinda.
“Ningependa
kutoa wito kwa wateja wetu kujiunga zaidi kwani zawadi bado zipo na pongezi kwa
waliojishindia. Zawadi hizi tunazozitoa ni sehemu ya mpango wa StarTimes
kurudisha fadhila kwa wateja wake kuwa waaminifu na kutuunga mkono tangu awali
tulipoanza kufanya kazi.
Tunafahamu kuwa hiki tunachokitoa hakitoshi hata
chembe lakini tunachoweza kuwaahidi ni kuwapatia huduma bora na nafuu kwa
asilimia mia moja.” Alihitimisha Hanif
Mbali
na kukabidhiwa kwa mshindi huyo, StarTimes pia walichezesha droo kumtafuta
mshindi wa nne wa pikipiki ambapo Bw. Samson Mollel, mkazi wa Arusha ambaye
amenunua king’amuzi cha kulipia cha NYOTA kinachouzwa kwa shilingi 34,000 siku
moja kabla ametajwa kuwa ni mshindi. (Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment