Maandamano yanaendelea kwenye mji mkuu wa Burundi Bujumbura kwa siku ya tatu kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu.
Watu wanachoma magurudumu ya magari na kuweka vizuizi huku nao polisi wakirusha vitoa machozi.
Maandamano hayo kwa mara ya kwanza, yamesambaa kwenda nje ya mji mkuu. Polisi wamezuia wanafunzi wa chuo kikuu kwenye mji ulio kati kati mwa nchi wa Gitega waliojaribu kuandamana kwenda mjini.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa karibu watu 25,000 wamekimbia nchi hiyo ndani ya majuma mawili yaliyopita, wakihofia kuongezeka kwa ghasia kabla ya uchaguzi mkuu unaokuja.
No comments:
Post a Comment