Mbunge wa zamani katika bunge la Afrika mashariki Francois Bizimana ameripotiwa kutekwa nyara siku ya jumapili mjini Bujumbura na watu wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na serikali.
Bizimana ni miongoni mwa viongozi wa upinzani nchini Burundi ambao wanampinga rais Pierre Nkurunziza.
Mwandishi wa BBC Robert Kiptoo anasema kuwa vyombo vya habari vinaripoti kuwa kiongozi huyo wa upinzani alitekwa na watu waliojihami.
Washirika wake pia wamekamatwa.

No comments:
Post a Comment