TANGAZO


Tuesday, April 7, 2015

Hoteli mpya ya New Pemba Seaview yafunguliwa Machomane, Pemba

Mwonekano wa Hoteli mpya ya New Pemba Seaview.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na wananchi wa Machomanne Chake Chake Pemba, kabla ya kuifunguwa hoteli ya Muwekezaji Mzalendo wa Pemba.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akihimiza jambo kabla ya kuifungua hoteli ya Mzalendo kisiwani Pemba, Halfan Hababu (Kidishi) kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, akiwa pamoja na viongozi mbali mbali wa Serikali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, akikata utepe kuashiria kuifungua rasmi hoteli inayomilikiwa na Mzalendo wa kisiwani Pemba, Halfan Hababuu (Kidishi), huko katika maeneo ya Machomanne Chake Chake Pemba.
Katibu Tawala Wilaya ya Chake Chake Mhe:Rashid Khadid akimuonesha waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Mohamed Aboud Mohamed, mazingira ya mji wa Chake Chake ukiwa juu ya hoteli ya Mzalendo wa Kisiwa cha Pemba, (Picha zote na Abdi Suleiman, PEMBA)

No comments:

Post a Comment