Kituo cha runinga cha Cinq Monde nchini Ufaransa, kinaendelea na harakati za kurejesha matangazo katika vituo vyake kumi na moja, baada ya watu wanaodai kuwa ni wanachama wa kundi la wapiganaji wa Islamic State kudukua matangazo yake.
Mkurugenzi wa kituo hicho amesema kuwa tayari wameanza kurusha matangazo yao, ila tu ni vipindi vilivyorekodiwa awali kwa sababu hawajafanikiwa kutatua udukuzi huo.
Awali katika ukurasa wa kwanza wa mtandao wake kulikuwa na bango la kundi lililojiita kundi lililojitenga la Mtandao likiwa na maandishi mimi ni wa kundi la Islamic state.
Wadukuzi hao pia wamechapisha nyaraka katika mtandao wa kijamii wa kituo hicho wakidai kuwa ni vitambulisho vya familia za wanajeshi wa Ufaransa wanaopambana na wapiganaji wa Islamic State.

No comments:
Post a Comment