Vinara wa ligi ya England Chelsea leo watashuka dimbani kucheza mchezo wao wa kiporo dhidi Leicester City.
Mchezo huu utachezwa katika dimba la King Power, Chelsea washuka dimbani katika mchezo huo wakiwa na alama 77 baada ya kushuka dimbani mara 33.
Huku Leicester wakiwa nafasi ya 17 kwa alama 31 wakihitaji ushindi ili kujiwekea nafasi nzuri ya kutoshuka daraja .
Bado kuna wasiwasi kama Chelsea wataweza mtumia mshambuliaji wao Diego Costa,Pia mshambuliaji Loicy Remy ataendele kukosa michezo ya ligi hiyo.
Kwa upande wa Leicester wachezaji David Nugent na Jeffrey Schlupp huenda wakaukosa mchezo huo kwa sababu ya maumivu.
No comments:
Post a Comment