TANGAZO


Monday, February 9, 2015

Wanawake wa Dodoma watakiwa kuchunguza Saratani ya matiti wapate kutibiwa

Mlezi wa Umoja wa Wanawake Tanzania [UWT] Haidaly Guramali akiwa pamoja na wataramu wa Magonjwa ya wanawake wa Ocen Road waliopo mjini Dodoma kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi wa Saratani ya Matiti wanawake zaidi ya 1500 unaofanyikia Nyerere Square kwa siku 5.
Wanawake wakazi wa manispaa ya Dodoma wakiwa Nyerere Square wakisubili kupatiwa uchunguzi wa saratani ya matiti chini ya wataaramu wa magonjwa ya wanawake toka Ocen Road ambapo upimaji huo utafanyika kwa siku 5. 
Mlezi wa UWT Haidaly Guramali akisalimiana na mmoja wa wanawake waliofika kufanyiwa uchunguzi wa Saratani YA Matiti katika viwanja vya Nyerere Square.
 Wanawake wakazi wa manispaa ya Dodoma wakiwa Nyerere Square wakisubili kupatiwa uchunguzi wa saratani ya matiti chini ya wataaramu wa magonjwa ya wanawake toka Ocen Road ambapo upimaji huo utafanyika kwa siku 5.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Fatma Ally akizungumza na wanawake waliokuwa wamekusanyika katika viwanja vya Nyerere Square kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa Saratani ya Matiti unaofanyika kwa siku 5 chini ya wataaramu wa magonjwa ya akina mama toka Ocen Road Dar es Salaam.

Na John Banda, Dodoma
WANAWAKE wametakiwa kupima saratani ya Matiti na shingo ya uzazi mapema kabla ya ugonjwa huo kufikia hatua mbaya ambayo si rahisi kutibika kama ilivyo kwa magonjwa ya malaria na Ukimwi.
Akizungumza wakati alipokuwa akizindua kampeni za upimaji wa saratani ya Matiti Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Fatma Ally kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni Mstaafu Chiku Gallawa amesema ugonjwa unaua wanawake wengi kuliko magonjwa mengine.
Mkuu wa Wilaya huyo alisema kwa kuwa wanawake wengi hawana utamaduni wa kupima afya zao wamekuwa wakijikuta tayari wameshaathika kwa kiasi kikubwa hali ambayo siyo rahisi kutibika hata wanapopelekwa Hosptalini.

Alisema ugonjwa huo ukigungulika katika hatua za awali unatibika hivyo ni jukumu la kila mwanamke kujitokeza na kupima ili atakapokutwa ana maambukizi ya awali aweze kuwahi kupata matibabu ambayo yanatolewa bure na Serikali.

“Kinamama wenzangu najua jinsi mnavyoweka neti kujikinga na mbu wa malaria na wengine wanaogopa vilusi vya ukimwi wakati ugonjwa unaowaua sana wanawake ni saratani ya matiti na kwa kuwa hapa kupima ni bure kila mtu akaje na wenzake 5 ili tuweze kusaidiana”, alisema Fatma.

Kwa upande wake Mlezi wa UWT wilaya ya Dodoma aliyefadhili Uchunguzi huo Haidaly Gulamali alisema aliamua kuufadhili umoja huo wa wanawake kutokana na wanawake wengi kutojua kama wana saratani ya matiti kutokana na kutokuwa na kawaida ya kupima afya zao.

Jumla ya wanawake 2000 wanatarajiwa kupima Saratani ya matiti unaoendeshwa na wataaramu wa magonjwa ya wanawake toka Hospital ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam utakaofanyika kwa siku tano zitakazoishia Ijumaa wiki hii.

No comments:

Post a Comment