TANGAZO


Wednesday, February 11, 2015

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wawatembelea Yatima wa Kituo cha Malaika Kinondoni Dar es Salaam

Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na mtoto Pendo Juma (kushoto)anaelelewa katika kituo cha yatima cha Malaika cha Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakiwa wamebeba mfuko wa mchele wakati baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho kuwasilisha msaada kwa niaba ya wafanyakazi wenzao ya vitu mbalimbali kama nguo, chakula na vitabu akiongozana nao kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia.
Mtoto Upendo Juma (kulia) anaelelewa katika Kituo cha yatima cha Malaika cha Kinondoni jijini Dar es Salaam akipokea sabuni za mche kwa niaba ya watoto wenzake wa kituo hicho kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kushoto) aliyekabidhi misaada hiyo kwaniaba ya wafanyakazi wenzake waliyochanga michango yao ya vitu mbalimbali kama nguo, chakula na vitabu kwa ajili ya watoto wa kituo hicho.
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa  wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba (wanne toka kulia) akizungumza na Mwendeshaji Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Malaika kilichopo kinondoni Jijini Dar es Salaam, Bi. Najma Manji(wa tatu toka kulia) wakati baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walipotembelea kituo hicho jana kuwasilisha misaada ya vitu mbalimbali kama nguo, chakula na vitabu kwa niaba ya wafanyakazi wenzao walivyochanga. Akishuhudia(wa tano toka kulia)ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia 
Watoto kutoka Kituo cha watoto yatima cha Malaika cha Kinondoni Jijini Dar es Salaam wakipokea nguo na sabuni kutoka kwa Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa  wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba (kulia) na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa  wa Kinondoni, Inspekta Eunice Muura(kushoto) msaada huo ulitolewa na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania (hawamo pichani) walipotembelea kituo hicho jijini Dar es Salaam jana kuwasilisha msaada wa vitu mbalimbali kama nguo, chakula na vitabu kwa niaba ya wafanyakazi wenzao.
Baadhi ya watoto  wa Kituo cha yatima cha Malaika cha kinondoni jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakati walipofika kituoni hapo jana kuwasilisha msaada wa vitu mbalimbali kama nguo, chakula na vitabu kwa niaba ya wafanyakazi wenzao walivyochanga kwa ajili ya watoto hao.

No comments:

Post a Comment