Makamo wa rais wa Marekani, Joe Biden, amesema Marekani iko tayari kuisaidia Ukraine kujihami dhidi ya wapiganaji wanaosaidiwa na Urusi.
Akizungumza kwenye mkutano mjini Munich, Ujerumani, kuhusu usalama wa Ukraine, Bwana Biden alisema Marekani inataka suluhu ya amani katika mzozo wa Ukraine.
Lakini alisema mara nyingi Rais Putin ameahidi amani huku akiendelea kuwapatia wapiganaji wanajeshi, vifaru na silaha.
Hapo awali, kiongozi wa Ujerumani, Angela Merkel, alionya kuwa Ukraine isipatiwe silaha - lakini alisema hakuna hakika kuwa juhudi za sasa za kutafuta amani zitafanikiwa.
Rais Putin amekanusha kuwa Urusi inataka vita - lakini kwa mara nyegine tena amelalamika juu ya vikwazo vilivowekwa na mataifa ya magharibi dhidi ya nchi yake.
No comments:
Post a Comment