TANGAZO


Saturday, February 14, 2015

Salva Kiir atabaki zaidi madarakani

Salva Kiir na Riek Machar
Serikali ya Sudan Kusini imefuta uchaguzi mkuu uliotarajiwa kufanywa mwezi wa Juni.
Msemaji wa serikali alieleza kuwa pendekezo la kurefusha uongozi wa Rais Salva Kiir kwa miaka miwili litapelekwa mbele ya bunge Jumaane.
Alisema kurefusha muhula wa Rais Salva Kiir kutaipa serikali muda wa kufanya mazungumzo ya amani na wapiganaji wa makamo wa rais wa zamani, Riek Machar.
Mapigano yameendelea Sudan Kusini ingawa yamefikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano mara kadha.
Mashirika ya misaada yameonya kuwa nchi hiyo, ambayo ilijitenga na Sudan mwaka wa 2011, inakaribia njaa.

No comments:

Post a Comment