Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akiongea na wananchi wa Kata ya Mbwala, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, hivi karibuni kabla ya kukabidhi vifaa tiba vitakavyotumika katika Zahanati mbalimbali wilayani humo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kushoto), akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Mbwala, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, Juma Ligomba, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba ambavyo vitatumika katika zahanati mbalimbali wilayani humo. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical inayojishughulisha na masuala ya Afya na Tiba, Peter Joseph Karia ambayo imechangia kufanikisha upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba vilivyokabidhiwa katika zahanati ya Nyamwage, Kata ya Mbwala hivi karibuni.
Wananchi wa Kijiji cha Nyamwage, Kata ya Mbwala, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, wakimkasikiza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid hivi karibuni kabla ya kukabidhi vifaa tiba vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani humo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (aliyevaa shati la batiki), akishirikiana na wananchi wa Kijiji cha Nyamwage, Kata ya Mbwala, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani kufungua kitanda kwa ajili ya akinamama kujifungulia hivi karibuni, wakati alipokabidhi vifaa tiba kwa ajili ya wilaya hiyo. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical, inayojishughulisha na masuala ya afya na tiba, Peter Joseph Karia ambayo imechangia kufanikisha upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba vilivyokabidhiwa katika zahanati ya Nyamwage, Kata ya Mbwala hivi karibuni.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, akimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical, inayojishughulisha na masuala ya afya na tiba, Peter Joseph Karia ambayo imechangia kufanikisha upatikanaji wa baadhi ya vifaa tiba vilivyokabidhiwa katika zahanati ya Nyamwage, Kata ya Mbwala, hivi karibuni.
Mmoja wa akina mama wakazi wa Kata ya Mbwala, Rufiji, akimshukuru Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid kwa kuwapatia vifaa tiba kwa ajili ya kuwalinda
na kuimarisha afya ya mama na mototo. (Picha
zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
Na
Eleuteri Mangi- MAELEZO
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid amekabidhi vifaa tiba vyenye thamani
ya sh milioni 23.8 ambavyo vitakavyotumika katika zahanati mbalimbali wilayani
Rufiji mkoa wa Pwani.
Vifaa
vilivyokabidhiwa ni pamoja na kitanda kimoja kwa ajili ya akina mama
kujifungulia chenye thamani ya sh. Milioni 1.5, vitanda 50 na magodoro manne.
Makabidhiano
hayo ya vifaa hivyo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika zahanati ya Nyamwage
iliyopo kata ya Mbwala wilayani Rufiji huku yakishudiwa na wananchi wa eneo
hilo wakiwa mashuhuda wa makabidhiano hayo.
Akikabidhi
vifaa hivyo, Dkt. Seif aliwaasa wananchi wanaotumia zahanati hiyo kuvitumia na
kuvitunza vizuri vifaa hivyo ili kupunguza tatizo la akina mama wajawazito
kupata adha wakati wa kujifungua na wagonjwa wengine wanakaopata huduma katika
zahanati hiyo.
Dkt.
Seif alisema kuwa vifaa hivyo vinatokana na moyo wa wanarufiji waishio jijini
Dar es salaam na marafiki wa Rufiji ambao wameanzisha mfuko wa Maendeleo wa
Wanarufiji unaolenga kuinua maisha ya wananchi wa wilaya hiyo katika kusimamia
upatikanaji wa huduma za jamii ikiwemo afya, umeme, upatikanaji wa maji safi na
salama, elimu, kilimo, biashara na ardhi.
Kuhusu
suala la umeme, Dkt. Seif alisema kuwa mpaka sasa wilaya ya Rufiji vipo vijiji
39 ambavyo tayari vimeunganishiwa huduma hiyo ambapo taendelea kusaidia
kuboresha vitu vingi akitolea mfano Nyamwage ilivobadilika na kuwa na maendeleo
makubwa kiuchumi.
Na
kwa upande wa huduma ya maji kwa wananchi wa Rufiji, Dkt. Seif alisema kuwa
kamati ya mfumko wa maendeleo Rufiji kwa kushirikiana na marafiki wa Rufiji
watachima visima zaidi ya 25 katika vijiji mbalimbali ili kuwapunguzia wananchi
adha ya upatikanaji salama na kutumia muda mwingi katika shughuli za kiuchumi
waweze kujiletea maendeleo yao kwa kushirikiana na Serikali.
Dkt.
Seif alibainisha kuwa umoja wa wanarujiji hao walifanya harambee mwaka jana
jijini Dar es salaam iliyoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe
Dkt. Mohamed Gharib Bilal ambapo zilipatika sh. Milioni 900 ambapo lengo la
harambee hiyo lilikuwa kukusanya sh. Milioni 1.5.
“Wenzetu
wamejitahidi wamefanikiwa kukusanya kiasi hicho katika harambee hiyo leo hii
wanarufiji tunapokea michango ya wenzetu wanaothamini afya zetu na maendeleo ya
wilaya yetu” alisema Dkt. Seif.
Aidha,
Dkt. Seif alisema kuwa mfuko huo umeanzishiwa akaunti yake ambapo michango yote
huwekwa pamoja na kamati husika inapanga ni vipaumbele vipi vifanyiwe kazi
kwanza na ni kwa eneo gani la wilaya na kwa wakati gani.
Naye
Mkurugenzi wa kampuni ya Giant Surgical and Pharmaceutical inayojishughulisha
na masuala ya afya na tiba Peter Joseph Karia alisema kuwa kampuni yake
imesukumwa na moyo wa kuwasaidia wanarufiji kwani yeye amesomea wilayani humo
hivyo kampuni yake inathamini na itaendelea kusaidia masuala ya kiafya ambayo
ndio kiini cha ufanisi wa maaenedeleo wilayani humo.
Kampuni
hiyo katika kufanikisha utoaji wa huduma bora za jamii imechangia na kutoa
vitanda 50, mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara na
kuahidi kutoa madawati 10 pamoja na pesa sh. Milioni 10.
Harambee
ya kusaidia Rufiji iliyofanyika jijini Dar es salaam ilifanikishwa na
kusimamaiwa na wanarufiji kwa kushirikiana na kampuni ya Giant Surgical and
Pharmaceutical na Jumuiya wa Kiislamu ya ISTIQAAMA.
No comments:
Post a Comment