TANGAZO


Wednesday, January 21, 2015

Wapiga kura wanavyowalaghai wabunge UG

Wapiga kura kwenye mkutano wa kisiasa nchini Uganda
Kiwango cha wapiga kura kuwalaghai wawakilishi wa bunge nchini Uganda ni cha kutisha.
Mwathiriwa wa hivi karibuni kulingana na jarida la Political Xtra ni mbunge wa Bubulo Mashariki Simon Mulongo.
Hivi ndivyo mbunge huyo alivyowashtumu walaghai hao katika mtandao wake wa facebook.
''Sifurahii tabia za baadhi ya raia kutoka masaba ambao wamekuwa walaghai.
Nimekuwa na visa kadhaa vinavyohusisha uongo kuhusu maiti zinazohitaji kusafirishwa kwa mazishi ya uongo ambayo yanahitaji usaidizi wangu.''wakati huu ilikuwa ni mtu anayejiita Mukasa kutoka Lwakhakha ambaye alidai amekwama huko Nakawa.
Alisema kuwa alitaka fedha za kulipia mahala pa kulala na nauli ardu nyumbani.
Kutoka kwa mtandao wake wa facebook,mtu huyo ni mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha kingston mjini kampala'',alisema Mulongo.''Hakuthibitisha kwamba alikuwa amekwama.
Wakati nilipompigia katika nambari ya usajili,alishindwa kujitetea alikuwa anatetemeka'',aliongezea.
Tafadhali ndugu zangu wa Bamasaba ,musichukulie usaidizi kutoka kwa wabunge kwa urahisi,.Wabunge wana uwezo wa kubaini uongo.Kwa kutumia vibaya ukarimu munaweza kuwaharibia wale wanaohitaji msaada huo.
Kulingana na Utafiti mpya kuhusu siasa za biashara,wabunge hulazimika kusimamia visa vingi vya mahitaji ya fedha kutoka kwa wapiga kura wao na kuwawacha wakiwa na madeni mengi.
Utafiti huo unasema kuwa kwa jumla wabunge hutumia shilingi millioni 4.6 kila mmoja wao kutoa usaidizi wa kifedha kwa wapiga kura wao kila wanapowatembelea katika maeneo bunge, huku kiwango cha chini wanachotumia kikiwa laki moja na kile cha juu kikiwa millioni 100.

No comments:

Post a Comment