TANGAZO


Sunday, January 11, 2015

Waja wazito waumia zaidi na Ebola


Mwanamke ashiriki kwenye kampeni ya kuhamasisha watu kujikinga na Ebola mjini Freetown

Kituo kipya cha matibabu kimefunguliwa Sierra Leone ili kushughulikia kutibu wanawake wajawazito.
Shirika la matabibu la kimataifa, MSF, linasema kuwa wajawazito ndio wako hatarini kabisa, kwa sababu virusi vya Ebola vinaingia kwenye mfuko wa mimba na kufanya mimba itoke.
Zahanati hiyo iko kwenye eneo lenye ebola nyingi katika vitongoje vya mji mkuu, Freetown.
Wanawake wanaambukizwa Ebola sana kwa sababu mara nyingi wao ndio wanauguza wagonjwa ndani ya familia.
Lakini haijulikani kwanini wanawake wajawazito wakipata ebola ni nadra kupona; na wakuu wa matibabu wanasema wanahitaji kufanya utafiti zaidi.
Watu zaidi ya 8,000 wamekufa kutokana na Ebola nchini Sierra Leone, Guinea na Liberia tangu ugonjwa huo kuanza mwaka mmoja uliopita.

No comments:

Post a Comment