TANGAZO


Tuesday, January 20, 2015

Viongozi Arsenal watembelea PSPF kwa lengo la kusaka fursa za mahusiano ya Kibiashara Tanzania

Mkurugenzi wa Mahusiano ya kimaendeleo wa Klabu ya Arsenal Bw. Sam Stone (kulia) akimkabidhi jezi ya timu hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu. Kushoto ni Bw. Daniel Willey, Meneja wa Mahusiano ya Kimaendeleo ya Arsenal. Maafisa hao wapo nchini kwa lengo la kukutana na wadau mbalimbali ili kufungua mahusiano ya kibiashara, katika mpango huo makocha wa timu hiyo na baadhi ya nyota waliowahi kuchezea timu hiyo watapata fursa kutembelea Tanzania. Klabu ya Arsenal ni kati ya klabu maarufu ulimwenguni ambayo inashiriki ligi maarufu duniani ya Barclyas 
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akimkabidhi zawadi  Mkurugenzi wa  Mahusiano ya kimaendeleo wa Klabu ya Arsenal Bw. Sam Stone (kulia) , kushoto ni  Bw. Daniel Willey, Meneja wa Mahusiano ya Kimaendeleo ya Arsenal. 
Mkurgenzu Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu (kushoto), akimkabidhi zawadi Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Bw. Imani Kajura ambaye ni mwenyeji wa maofisa kutoka klabu ya Arsenal ambao wapo nchini kwa ajili ya kukutana na wadau mbalimbali kwa lengo kufungua mahusiano ya kibiashara.

No comments:

Post a Comment