TANGAZO


Wednesday, January 14, 2015

Simba ilipoifunga Mtibwa Sugar Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Aman na kunyakua kombe la Ubingwa

*Simba yaipiga Mtibwa Sugar kwa penalti 4-3

Mshambuliaji wa timu ya Simba Ramadhani Singano Messi, akimpita beki wa timu ya Mtibwa Sugar wakati wa mchezo wao wa Fainal ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika usiku wa kuamkia leo uwanja wa Amaan, Timu ya Simba imeshinda kwa penenti 4--3.
Wapenzi wa mchezo wa mpira Zanzibar wakifuatilia mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi liofanyika usiku huu uwanja wa amaan Zanzibar timu ya Simba imeshinda mchezo huo na kuwa Bingwa kwa mwaka 2015 bingwa Mapinduzi Cup.
Mshambuliaji wa timu ya Simba Emanuel Okwi, akimpita beki wa timu ya Mtibwa wakati wa mchezo wao wa fainali ya Kombre la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan, usiku wa kuamkia leo.
Mshambuliaji wa timu ya Mtibwa akimpita beki wa timu ya Simba katika mchezo wa fainali ya Kombev la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa amaan Zanzibar usiku wa kuamkia leo.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiangalia mchezo kati ya timu hizo, akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa Serikali na Vyama vya Michezo.




Kocha wa Simba akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko.


Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa na majonzi wakati wa mchezo wa timu ya Mtibwa kuwa sare wakati wa kipindi cha pili kumaliziki hawaamie kama mchezo umemalizika kwa sare ya bila kufungana na kupigiana penenti Simba imeshinda 4 na kukosa moja wakati Mtibwa wameshinda 3 na kukosa mbili. 
Wachezaji wa Timu Simba wakishangilia Ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi baada ya kushinda Mchezo wa Fainali na Timu ya Mtibwa kwa kuifunga 4--3. 
Kipa wa timu ya Simba Ivon Mapundu akijaribu kudaka bila mafanikio moja ya penenti katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi. Simba imeshinda kwa penenti 4--3
Kipa wa timu ya Mtibwa Sugar, Said Abdallah akidaka bila mafanikio moja ya penenti katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi. Katika mchezo huo, Simba imeshinda kwa penenti 4--3. (Picha zote kwa hisani ya ZanziNews Blog)

No comments:

Post a Comment