TANGAZO


Monday, January 19, 2015

Mume akiri kumchinja mkewe London

Naveen Ahmed anatarajiwa kuhukumiwa kwa mauaji tarehe 28 Januari
Mwanamume mmoja amekiri kumchinja na kisha kumkatakata mkewe katika nyumba yao mjini London.
Naveed Ahmed, mwenye umri wa miaka 41, alikiri makosa yake ya kumuua mkewe ambaye ni mama wa watoto wake wawili, Tahira Ahmed, 38.
Mwili wa Bi Ahmed ulipatikana na polisi tarehe 27 mwezi Mei baada ya majirani kuripoti kwamba walisikia wawili hao wakigombana.
Uchunguzi wa kifo cha mwanamke huyo ilisema kuwa alipatikana akiwa amekatwa mikono, kudungwa kisu na kisha kukatwakatwa.
Tahira Ahmed alipatikana akiwa amechinjwa nyumbani kwao mjini London
Bwana Ahmed anatarajiwa kuhukumiwa tarehe 28 mwezi huu katika mahakama aya Old Bailey.
Inaarfiwa jaji amemuonya kwamba huenda akafungwa jela kwa mauaji hayo.
Awali Ahmed alikana mauaji ya mkewe wakati kesi ilipoanza kusikilizwa mwezi Oktoba.

No comments:

Post a Comment