TANGAZO


Wednesday, January 7, 2015

Muasi Dominic Ongwen ajisalimisha

Inaarifiwa Kamanda Ongwen alikuwa naibu wa Joseph Kony ambaye ndiye kiongozi wa LRA
Dominic Ongwen, mmoja kati ya makamanda aliyekuwa na cheo kikubwa katika jeshi la waasi wa Uganda Lord Resistance Army (LRA) ambaye pia alikuwa mtu wa karibu sana na Joseph Kony, amejisalimisha kwa kikosi cha jeshi la Marekani kilichoko Afrika ya kati.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa kikosi cha Marekani nchini humo.
Dominic alitekwa nyara na LRA alipokuwa na umri wa miaka 10, na alikuwa akipanda vyeo katika jeshi hilo la waasi na amekuwa akisakwa na mahakama ya uhalifu wa kivita kwa makosa kadhaa yakiwemo ya mauaji ,uporaji,pamoja na utumikishaji.
Msemaji wa jeshi aliambia BBC kwamba wanajeshi wamemtembelea Dominic Ongwen, ambaye alijislaimisha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kuwema kumtambua.
Kiongozi wa waasi wa Uganda LRA,Joseph Konyi
Mahakama ya kimataifa ya ICC, inamtaka bwana Ongwen kwa ajili ya kumfungulia mashitaka ya makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Lakini serikali ya Uganda imesema inataka kumfungulia mashitaka nchini Uganda.
Msemaji wa serikali, Ofwono Opondo aliambia BBC kua Ongwen anatarajiwa kufikishwa Uganda mwishoni mwa wiki,ambapo atafunguliwa mashtaka rasmi.
Kundi la LRA lilitenda uhalifu mkubwa dhidi ya bindamau hasa kwa kuwatumia watoto katika vita, Kaskazini mwa Uganda, na katika mataifa jirani huku likiwalazimisha watoto wavulana kupigana pamoja na kuwatumia wasichana kama watumwa wa ngono.
Marekani kwa mara ya kwanza ilituma wanjeshi 100 nchini Uganda mwaka 2011 kuwasaidia maelfu ya wanajeshi wa Afrika katika kuwaska makamanda wa LRA.
Dominic Ongwen anatazamiwa kama naibu wa kiongozi wa LRA Joseph Kony.

No comments:

Post a Comment