Kikosi cha timu ya Shaba wakipasha wakisubiri kukagulia na kusalimiana na meni rasmin wa mchezo huo wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar. (Picha zote kwa hisani ya ZanziNews)
Kikosi cha timu ya Yanga wakipasha wakisubiri kukagulia na kusalimiana na meni rasmin wa mchezo huo wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Wachezaji wa timu ya Yanga wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Shaba kabla kuaza kwa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.Katika mchezo huo Yanga imeshinda bao 1--0.
Kikosi cha timu ya Yanga kilichomaliza michezo yake bila ya kufungwa katika kundi lao na kujichukulia pointi zote 9, katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kikosi cha Timu ya Shaba (Wazee wa Dago) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza mchezo wao na Yanga kukamilisha ratiba ya Kombe la Mapinduzi hatua za makundi, ilikubali kipigo cha bao 1--0 kutoka kwa timu ya Yanga.
Kizaazaa golini kwa timu ya Shaba wakati wa mchezo wao na timu ya Yanga kuwania Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa amaan.
Wapenzi wa mchezo wa mpira Zanzibar wakifuatilia mchezo kati ya Yanga na Shaba uliofanyika uwanja wa Amaan.Timu ya Yanga imeshinda 1--0.
Waandishi wa habari za michezo kutoka magazeti mbalimbali wawakiripoti mchezo huo wa Shaba na Yanga kupitia katika simu.
Wachezaji wa timu ya Yanga na Shaba wakiwania mpira katika mchezo wa kuwania Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga Danny Mruwanda akiweka jaro golini kwa timu ya Shaba huku beki wa timu ya Shaba Juma Mwalim, akiwa tayari kumzuiya asilete balaa golini kwao.
Golikipa wa timu ya Shaba Bakari Hassan akiokoa mpira wa krosi uliopigwa na mshambuliaji wa timu ya Yanga Saimon Msuva, huku wachezaji wa Yanga wakiwa wamemzongea.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga Mbrazil Coutihno akimpita beki wa timu ya Shaba Robert Daniel katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya Yanga imeshinda bao moja kupitia mshambuliaji wake huyo Mbrazil, katika dakika ya 86 ya mchezi kipindi cha pili
Kasheshe langoni kwa Shaba.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakiishangilia timu yao wakati ikicheza na timu ya Shaba (Wazee wa Dago), mchezo uliofanyika uwanja wa amaan.
Purukushani langoni kwa timu ya Shaba.Mrisho Ngassa wa Yanga akikimbia na mpira.
Golikipa wa Shaba, akivuliwa glovu na Msuva baada ya kuumia.
Golikipa wa timu ya Shaba, Shamte, akidaka mpira.
Msuva akitafuta mbinu ya kumtoka mchezaji wa timu ya Shaba.
Purukushani langoni kwa timu ya Shaba ya Pemba.
Wapigapicha wa Magazeti mbalimbali na blogu wakiwa Uwanja wa Aman wakati wa mchezo huo.
Mchezaji Andrey Continho (mbele), akishangilia na wenzake, goli aliloifungia timu yake ya Yanga dhidi ya Shaba ya Pemba, katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi, uliochezwa Uwanja wa Aman, mjini Unguja usiku wa kuamkia leo.
Mchezaji Andrey Continho (mbele), akishangilia na wenzake, goli aliloifungia timu yake ya Yanga dhidi ya Shaba ya Pemba, katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi, uliochezwa Uwanja wa Aman, mjini Unguja usiku wa kuamkia leo. Katika mchezo huo, Yanga ilishinda bao 1-0.
No comments:
Post a Comment