TANGAZO


Thursday, January 22, 2015

Halmashauri ya Wilaya ya Momba yahaidi kuunda Saccoss ya Vijana kwa maendeleo ya Vijana

Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Momba Bw. Severine Chamkaga akifungua semina ya Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za Maisha na Ujuzi jana katika Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya. Wa pili kulia ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa, wa kwanza kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga, na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa akitoa mada wakati wa semina ya Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za Maisha na Ujuzi jana katika Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya.
Ofisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada wakati wa semina ya Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za Maisha na Ujuzi jana katika Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya.
Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada wakati wa semina ya Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Stadi za Maisha na Ujuzi jana katika Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya.
Kijana Adam Zacharia Kinyakile (wa pili kulia), anayeinua vipaji vya vijana na kutengeneza ajira kwa vijana katika fani ya ufundi gereji Mji wa Tunduma Wilaya ya Momba akiwaonyesha maafisa waliomtembelea katika shughuli zake “Mobile Garage” aliyoitengeneza mwenyewe kwa kutumia vyuma chakavu inayoitumia kufanyia kazi za gereji mahali popote anapohitajika. Kushoto ni Mwenzeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamduni na Michezo Bibi Ester Riwa pamoja na timu kutoka Wizara hiyo.
Ofisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Amina Sanga wa pili kushoto (waliokaa) akizungumza na Vijana wa kikundi cha Matunda Wilaya ya Momba walipowatembelea wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Vijana Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na wa pili kushoto ni Mwenzeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Ester Riwa. (Picha zote na Genofeva Matemu – Maelezo. Momba, Mbeya)

No comments:

Post a Comment