Timu ya Gabon ilianza vyema kampeni yake ya kulinyakua kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuishinda Burkina Fasso na kupanda katika kilele cha kundi A.
Mchezaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubemeyang aliiweka Gabon kifua mbele kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.
Burkina Fasso walikuwa hatari kwa kipindi kirefu cha mechi hiyo kupitia wachezaji Vitesse Arnhem na mchezaji wa Chelsea anayecheza kwa mkopo Betrand Traore wakishindwa kumfunga mlinda lango Didier Ovono katika vipindi vyote viwili.
Katika mechi kati ya waandalizi wa dimba hilo Equitoial Guinea na Congo ,Thievy Bifouma alifunga bao la muda wa lala salama na hivyobasi kuinyima ushindi timu hiyo ya nyumbani katika mechi iliochezwa mbele ya mashabiki wengi katika uwanja wa Bata.
Mchezaji wa Middlesbrough Emilio Nsue aliiweka Equitorial Guinea kifua mbele katika dakika ya 16 licha ya kuonekana kwamba alikuwa ameotea.
Francis N'ganga alipiga mlingoti wa goli huku Congo wakidhibiti mpira na kufanya mashambulizi chungu nzima katika kipindi cha pili kabla ya mshambuliaji wa West Brom Thievy Bifouma kufunga katika eneo la hatari.
Congo ingeshinda mechi hiyo lakini Dominique Malonga alikosa bao la wazi.
No comments:
Post a Comment