TANGAZO


Tuesday, January 6, 2015

Chanjo dhidi ya Ebola yatolewa

Chanjo dhidi ya Ebola itapelekwa nchini Liberia,Sierra Leone na Guinea
Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Oxford wameaza kutoa chanjo dhidi ya Ebola kwa Watu waliojitolea.
Majaribio haya yanahusisha Watu 72 wenye umri wa kati ya miaka 18-50.
majaribio ya awali yaliyofanywa kwa Nyani yalionesha ufanisi wa chanjo ya Ebola.
Watu waliojitolea chuoni hapo ni binaadamu wa kwanza kupata chanjo hiyo.
Dokta Matthew Snape kutoka idara ya Chanjo chuo cha Oxford amesema mpango huu unalenga kuwapa chanjo washiriki wote ndani ya mwezi mmoja.
Majaribio haya yanalenga kuelewa usalama wa Chanjo hiyo.
Waratibu wa mpango wa majaribio ya chanjo dhidi ya Ebola wamesema chanjo hiyo haisababishi mtu aliyeipata kuathiriwa na Ebola.
Wataalam wa maswala ya chanjo kutoka Kampuni ya Johnson and Johnson wamesema wana matumaini kuwa watafanya majaribio ya awamu ya pili barani Afrika na Ulaya ndani ya miezi mitatu kisha Chanjo hiyo itapatikana kwa ajili ya matumizi nchini Liberia, Guinea na Sierra Leone katikati ya mwaka huu.

No comments:

Post a Comment