Pages

Thursday, January 29, 2015

Bungeni leo: Halmashauri zahimizwa kuanzisha redio za kijamii

Na Lorietha Laurence-Maelezo

Naibu Waziri Nkamia 
HALMASHAURI za Wilaya na miji zimehimizwa kuanzisha vyombo vya habari vya kijamii ili kuwawezesha wananchi kupata habari kwa haraka zaidi.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni  na Michezo  Juma Nkamia alipokuwa akijibu swali la Mhe. Muhammad Sanya kuhusu  bei ya magazeti kuwa juu na hivyo kupelekea wananchi kukosa taarifa muhimu.

Mhe. Nkamia alikiri kuwa ni kweli bei za magazeti nchini ni kubwa na hiyo inatokana na gharama kubwa za uzalishaji, uendeshaji pamoja na usambazaji,  hivyo vyombo vya habari vya kijamii vitakuwa mbadala mzuri wa wananchi kupata habari.

“Ni vizuri halmashauri zikaanzisha vyombo vya habari vya kijamii ili kurahisisha upataikanaji wa habari kwa wananchi hususani wale walioko vijijini ambao wengi wao hutegemea vyombo hivyo kupata taarifa” alisema Nkamia.

Alisema iadha   vyombo vya habari vya kijamii husaidia sana  kutoa taarifa muhimu kwa jamii husika kwa wakati bila ya kujali faida kwa kufuata taratibu na sheria za utangazaji zilizowekwa na serikali.

Pia aliwaomba waandishi wa habari wazingatie maadili ya kazi zao ili kuepusha kufungiwa kwa magazeti pale inapoonekana vyombo hivyo vimekiuka na kwenda kinyume na sheria na taratibu zinazosimamia vyombo vya habari nchini.

No comments:

Post a Comment