TANGAZO


Tuesday, January 13, 2015

AFCON-Timu za kundi A zapasha misuli

Timu zinazoshiriki michuano ya kombe la Afrika toka kundi A ni Congo, Gabon na Burkina Faso na wenyeji Equatorial Guinea zinatofautiana kwa ubora katika viwango vya dunia vya Fifa
Mapema miaka ya sitini katika orodha ya Fifa ni alama tatu pekee zilizotofautisha timu hizo za kwanza.
Equatorial Guinea ikiwa imeorodheshwa nambari 181 katika orodha ya Fifa, ndio mwenyeji wa michuano hii.
Gabon haikupoteza katika michuano ya kufuzu lakini ilishinda mchezo mmoja tu katika michuano iliyochezwa ugenini maana kwamba timu huyo itamtegemea sana mshambuliaji wake Pierre-Emerick Aubameyang ambae atakua na mzigo wa kuibeba timu hiyo.
Jonathan Pitroipa ana mzigo mkubwa kuibeba timu ya Burkina Faso
Kwa upande wa Burkina Fasso watamtegemea winga wao mashuhuri Jonathan Pitroipa katika kuipa mafanikio timu hiyo.
Wakiwa wanajulikana kwa jina la utani Mashetani wekundu, Congo ndio wageni sana wa hivi karibuni katika michuano hio. Kocha wao ni Wily Claude LeRoy anaweza kuwawezesha kufanya vizuri hasa baada ya kuwabandua mabingwa Nigeria katika michuano ya kufuzu.
Wenyeji Equatorial Guinea walifanikiwa kufika robo fainali kwenye michuano iliyopita na mashabiki wao wana matumaini kwamba watafika mbali sababu wao ndiyo wenyeji.

No comments:

Post a Comment