TANGAZO


Tuesday, January 20, 2015

AFCON: Ebola yadhibitiwa katika michuano

Equitorial Guinea
Rais wa Shirikisho la Soka nchini Equatorial Guinea Andres Jorge Mbombio amesema kuwa athari ya ugonjwa wa Ebola nchini humo imedhibitiwa.
Polisi na mashabiki walipamabana na kuzua vurugu baada ya uchunguzi wa ebola kuwachelewesha mashabiki kuingia uwanjani kushuhudia mechi ambayo Zambia ilitoka sare ya 1 -1 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Ijapokuwa wakati wa kusubiri kuingia uwanjani, Mbombio anadai tishio la ebola lilidhibitishwa.
Alisema "wakati sisi tuliamua kuandaa mchuano huu, tulichukua hatua kamili za kuzuia ugonjwa huu, tunajivunia na kwa sasa tunataka kuwaza tu kandanda"
Equitorial Guinea
Kulikuwa na ulinzi mkali kabla ya mechi ya Zambia na Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo
Equatorial Guinea wameandaa mchuano huu baada ya ombi la Morocco kuhairisha mchuano huo kutupiliwa mbali na shirikisho la kandanda la Africa (CAF) mnamo November mwaka jana.
Mashabiki wanahitajika kusafisha mikono yao kwa kutumia sabuni ya aina ya Gel wanapoingia uwanjani, msimamo ambao umesababisha foleni ndefu.
Equitorial Guinea
Mbombio anasema hataki suala la Ebola kutawala mchuano huo na kubadili lengo la mchuano huu mbali na mashindano.
"Kila mtu alisema kuwa Ebola ni changamoto kubwa kwa mashindano haya. Na ni ukweli ni hatari, Lakini tuliweza kudhibiti," aliongeza.
"Sisi tumepewa nafasi ya kufurahia soka. Ni lazima kusahau matatizo yanayohusiana na Ebola."

No comments:

Post a Comment